DP Financial and Marketing Services

Tuesday, May 12, 2015

SAFARI LAGER WEZESHWA INATARAJIA KUTOA RUZUKU KWA WAJASIRIAMALI

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager inatarajia kukabidhi ruzuku kwa wajasiriamali waliopita katika programu ya Wezeshwa na Safari Lager IV.
Zoezi hili limehusishwa wataalamu wenye uwezo na uzoefu mkubwa katika kushauri na kusaidia ukuzaji wa sekta ya biashara ndogo na kubwa(TAPBDS CO. LTD). Wajasiriamali wanaopewa ruzuku ni wale waliopitishwa katika mafunzo ya kukuza nakuendeleza biashara zao ili kuleta chachu katika biashara zao na zile zinazowazunguka.
Bi Edith Bebwa aliyataja majina ya washiriki wataopata ruzuku hizo na maeneo amabayo shughuli ya ugawaji ruzuku itafanyika na tarehe ya ugawaji ruzuku kwa kuzingatia maeneo:
1.Mbeya ni Mei 16, 2015, New City Pub bendi ya TOT itatumbuiza
2.Mwanza ni Mei 23,2015,Uwanja wa furahisha bendi ya Zebedaki itatumbuiza.
3. Arusha ni Mei 30,2015, uwanja wa lenana Bar bendi ya Vibration itatumbuiza
4.Dar es salaam ni Juni 7, viwanja vya Leaders, bendi ya twanga pepeta itatumbuiza.
Pichani ni Bi Edith Bebwa(Meneja wa bia ya Safari Lager)na Bw. JOseph Migunda (Mkurugenzi kampuni ya TAPBDS CO.LTD) katika matukio mbalimbali walipokuwa wakiongea na waandishi wa habari na kuonesha vifaa vilivyonunuliwa.




https://www.facebook.com/TapbdsCoLtd

No comments:

Post a Comment