DP Financial and Marketing Services

Wednesday, November 23, 2011

Kanuni Za Kushiriki

1. Programu ya Wezeshwa iko wazi kwa Mtanzania yeyote mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 40 na awe anaishi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2.Nakala ya Kitambulisho cha mshiriki lazima kiambatanishwe na fomu ya usajili.

3.Ushiriki ni wa hiari na utanzingatia kanuni na maelekezo ya Programu.

4. Ukusanyaji wa fomu za programu utamalizika tarehe 15 February 2013, na fomu zote za ushiriki lazima zirudishwe katika vituo vilivyopangwa kabla ya saa 11 jioni ya siku hiyo.

5. Kampuni ya Tanzania Breweries Ltd haitawajibika kwa upotevu wa fomu za ushiriki au nakala za nyaraka zinazohusu programu hii.

6. Fomu ambazo hazijakidhi vigezo vilivyowekwa hazitazingatiwa.

7. Ni lazima mshiriki awe anaendesha na kusimamia biashara yake kwa muda wote.

8.Vigezo na masharti kuzingatiwa,Uamuzi wa majaji wa Programu hii ni uamuzi wa mwisho.

9. Kwa kukubali kushiriki na Programu hii ya TBL ina haki ya kutoa matangazo magazetini, kuchapisha majina na picha za 

washiriki na washindi wa shindano na pia kufanya nao mahojiano bila malipo ya ziada.

10.Waratibu wa Programu ya Wezeshwa wataendelea kukagua maendeleo ya biashara zinazoendeshwa na washindi pale 

itakapo lazimu kwa angalau kipindi cha miaka mitano (5).

11. Kanuni za ushiriki hazitabadilishwa wakati wa Programu.

Safari Lager Wezeshwa

Safari Lager yazindua Wezeshwa 
Usinduzi leo tarehe 23 november TBL, Kushoto ni mienja masoko wa tbl Mamongae Mahlare, Katikati Brand Manager wa safari lager Oscar Shelukindo na kulia ni Zozimiki Kimati kwenye uzinduzi wa program ya Wezeshwa na Safari Lager. 

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo Imezindua rasmi kampeni ya aina yake ya kuwatafuta na kuwawezesha wajasiriamali wadogowadogo katika shindano la wezeshwa na Safari Lager ambalo linaweza kumpatia mtu yeyote ruzuku ya kusaidia kuona njia ya mafanikio katika maisha yake. Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema Bia ya Safari Lager imezindua program hiyo ya wezeshwa ili kuwasaidia wamiliki wa biashara ndogondogo na za kati kukuza biashara zao,kuweza kuajiri zaidi ,kupata faida zaidi na pia kusaidia jamii yao. Alisema program ya Wezeshwa na Safari lager itatoa ruzuku yenye thamani ya jumla ya Tsh Milioni 200 kwa kuwawezesha wafanyabiashara watakaoingia na kufuzu vigezo vya program hii.Uwezeshwaji utakuwa kwa kupewa vitendea kazi muhimu vinavyohitajika ili kukuza biashara zao. Alisema zoezi hili litawahusu wafanyabiashara wenye ueledi wa uchapa kazi,wanaomiliki biashara binafsi na atakaeweza kusaidia jamii inayomzunguka. Kwa taarifa zaidi kuhusu program hii ya wezeshwa na Safari Lager unaweza kutembelea kiwanda chochote cha Tanzania Breweries Ltd ,Bohari kuu au wauzaji wa jumla na kuchukua fomu ya usajili au unaweza kutembelea tovuti ya www.wezeshwa.co.tz kisha jaza fomu hiyo na ipeleke katika kiwanda cha TBL hapa nchini au tuma barua pepe kwenda info@wezeshwa.co.tz