DP Financial and Marketing Services

Wednesday, July 15, 2015

KUJITAMBUA KAMA KIJANA.

Kujitambua ni ile hali ya mtu kujijua au kujielewa yeye ni nani, ana thamani gani, na umuhimu wake katika jamii anayoishi. Ni kuwa na uwezo wa kujua au kuelewa vipaji mbalimbali ambavyo Mungu amekujalia na uwezo wako wa kufanya mambo mbalimbali.Baadhi ya vipaji ni kama kuimba ,kufundisha ,uongozi,ufundi,biashara n.k

Pia kuelewa udhaifu ulionao kama binadamu na hivyo kujiepusha kuwa chanzo au chachu ya migogoro katika jamii unayoishi.Baadhi ya madhaifu ni :Hasira ,umbea,gubu,kisirani,ufitini,n.k

Ni kuwa na uwezo wa kuelewa nafasi yako na umuhimu wako katika jamii unayo ishi.Ni muhimu kutambua jamii inakuelewaje,una hekima au hapana;Ni kuwa na uwezo wa kuchambua malengo yako ya maisha na kuona kwamba ni halisi yanawezekana au hapana pamoja na kujiwekea mikakati ya kufanya ufanikiwe.

Ni kuwa na uwezo wa kutambua mambo yanayo kuogopesha katika maisha yako na sababu zake mfano:unaogopa kifo na kwanini unaogopa;Kuwa na upeo wa kuchambua aina ya watu unaopenda kuwa nao,wakiwa marafiki.Na kujaribu kujiuliza kila wakati,Je?marafiki ulionao ni wa sifa hizo?

Kwa kifupi naweza kusema kujitambua ni hali ya kuwa na ufahamu wa nini kuhusu wewe.Hali yako,umuhimu wako,malengo yako,hatima yako, changamoto zako, nk, hayo yote yanakuwa wazi kwako kwa kujitambua.
Reality  vs  Imagination.

No comments:

Post a Comment