SAFARI LAGER YATOA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI
Kampuni ya bia Tanzania (TBL) imetoa mafunzo kwa wajasiriamali 52 kutoka
mikoa mbalimbali ambao ni wa Shindano la safari
lager wezeshwa. Mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 13 - 17 mwezi Aprili
2015 yalifanyika kwenye mikoa ya Dar es salaam, Arusha, Mbeya na Mwanza yalilenga
kuwapa mbinu za kukuza na kuendeleza bisahara zao.
Safari
lager wezeshwa ni shindano liliyoanzishwa na kudhaminiwa na kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager. Shindano hili linaratibiwa na
kampuni ya Tanzania Association of Professional Business Development Providers
(TAPBDS) ambao ni wataalamu
waliobobea kwenye kutoa ushauri na mafunzo ya kuanzisha na kukuzuza biashara. Shindano
lilihusisha mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani. Shindano hili limelenga
kutoa ruzuku ya vifaa kwa wajasiriamali wadogo nchini Tanzania ili kusaidia
kukuza biashara zao.
Mchakato
wa kuwapata washindi hawa ulihusisha hatua zifuatazo;
1. Kupitia fomu za washiriki wote. Jumla ya wajasiriamali 3500 nchi nzima walijitokeza na kujaza fomu za
ushiriki, fomu hizo zilipitiwa na timu ya wataalamu kutoka TAPBDS Co. Ltd
ambapo washiriki 111 walikidhi vigezo kwa mujibu wa taarifa zao na kufanikiwa
kuingia hatua ya pili ya pili ya shindano.
2 Kuwatembelea wajasiriamali. Hatua iliyofuata ilikua ni kuwatembelea wajasiriamali wote waliovuka
hatua ya kwanza ili kujiridhisha kama walichokiandika kuhusu biashara zao ni
sahihi na kuhakiki umiliki wao kwenye biashara walizoombea ruzuku.
3. Mafunzo na ugawaji wa vyeti vya ushiriki.
Baada ya kuwatembelea wajasiriamali 111 waliovuka hatua ya awali,
wataalamu walipitia ripoti za uhakiki huo na kisha kupata wajasiriamali 52
ambao walifanikiwa kuingia hatua ya mafunzo ambayo pia yaliendeshwa na wataalamu kutoka TAPBDS Co. Ltd. Kanda ya kaskazini ilitoa washindi 21, kanda
ya ziwa washindi 10, Kanda ya kusini magharibi washindi 12, na kanda ya
mashariki na pwani washindi 9. Baada ya mafunzo wajasiriamali walikabidhiwa
vyeti vya ushiriki wa mafunzo.
Wajasiriamali wakiwa katika Picha ya Pamoja baada ya Kutunukiwa Vyeti vya ushirikiwa Programu ya Safari Lager Wezeshwa.
Mbali na mafunzo washindi hao walipata wasaa wa kubadilishana uzoefu,
kujadili changamoto mbalimbali za kibiashara, kutangaza biashara zao wakati wa
mafunzo na pia walitembelea viwanda vya bia vya TBL kwenye mikoa hiyo.
Baada ya kukamilika kwa mafunzo wajasiriamali walirejea kwenye mikoa yao
wakisubiri tarehe ya kukabidhiwa vifaa vyao kama ruzuku kwa ajili ya kukuza
biashara zao.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
No comments:
Post a Comment